KATIBA YA KIKUNDI CHA AGROBUSINESS
1. UTANGULIZI
(a)Hiki ni kikundi kilichoundwa na watu wapatao kumi (10), kikundi hiki kimeanzishwa tarehe 30
March 2016 eneo la Njiapanda ya Himo.
(b) Jina la kikundi ni “AGROBUSINESS GROUP"
2. MADHUMUNI YA KIKUNDI
Ni kufanya shughuli za uwekezaji ktk kilimo kwa pamoja ili kujiongezea kipato.
3. UANACHAMA
Mwanachama ni mtu yeyote mwenye akili timamu, mwenye mwelekeo wa mawazo yanayo fanana na
aliyeshiriki kuanzisha chama au kujiunga baadaye kwa kulipa kiingilio na kununua shares. Kuhudhuria
mikutano na anatimiza masharti ya chama kwa mujibu wa katiba hii.
4. KUPOTEZA UANACHAMA
(i) Mwanachama atapoteza uanachama iwapo atashindwa kutoa kiingilio na sehemu ya mtaji ambazo ni
Tshs (150,000/=) kwa miezi mitatu mfululizo kikundi kinapoanzishwa bila taarifa wala sababu za
msingi.
(ii) Kutohudhuria kwenye vikao kwa muda wa miezi mitatu mfululizo bila taarifa yoyote. Hivyo
atarudishiwa kiingilio chake, na ada aliyotoa wakati wa uanachama wake. Maana huwezi wekeza hela
kama mtu hajakubaliana na wazo hata kwa simu inatosha
5, MICHANGO
(a) Kiingilio ni Tshs. (20,000/=) mwanachama atalipa tu mara baada ya kujiunga ili kuchangia usajili
kikundi kama kampuni, Kuingia ktk mradi wa kikundi kila mwanachama atachangia kiasi cha sh
(150,000/) kama mtaji Ili mradi uanze
(b) Shares itakayolipwa na mwanachama kila mwezi itakuwa Tshs. (100,000/=) ktk kipindi cha kulima
Kiasi hiki kitabadilika kutegemea na mapendekezo ya wanachama kama itabidi kulingana na mtaji
kwa zao husika.
(c) Mradi ukipata dharura isipotosha akiba iliyopo kila mwanachama atachangia na asiyeweza
atakopeshwa au kusaidiwa hadi atakapotoa au kukatwa kwenye mgao
6. VIONGOZI
(1) Kikundi kitakuwa na viongozi wafuatao
(a) Mwenyekiti
(b) Katibu
(c) Mweka Hazina
(d) Meneja masoko na manunuzi.
(2) Madaraka na wajibu wa viongozi
(a) Wajibu wa Mwenyekiti:
. Atakuwa ni kiongozi wa watu wote. Atakuwa na kura ya uamuzi (turufu) iwapo
. kwenye uchaguzi kura zimelingana
. Kuwajibisha wale watakao kosa nidhamu.
. Kuhakikisha nidhamu inatawala wakati wote ndani ya chama
(b) Wajibu wa Katibu
. Kuandika na kutunza kumbukumbu zote za mikutano
. Kutayarisha minutes za mikutano
. Kupanga na kutoa taarifa za mikutano
(c) Wajibu wa Mhazini
. Kupokea na kutunza fedha za kikundi hiki
. Kuweka kumbukumbu za mahesabu na malipo
( c) Muda wa uongozi
Viongozi watakaa madarakani kwa muda wa miaka miwili
7. MASHARTI MENGINE
(a)Mwanachama akichelewesha kutoa mchango wa mwezi atalazimika kulipa faini ya Tshs 3000/=
(b) Mwanachama akitoka kwenye chama kwa hiari yake, anaweza uza shares zake kwa wanachama au
mtu wa nje baada ya wanachama kumkubali, au kusubiri hadi zizalishe alipwe mgao wake
(c) Mwanachama akifariki kikundi kitawarudishia aidha shares au gawio la mapato warithi
ataowaandika kwenye form ya kujiunga.
8. MGAO WA MAPATO
Mazao yakiuzwa hela itahifadhiwa bank na kwa pamoja wanachama wataamua
(1) Mradi uendelee kwa zao hilo au jingine
(2) Mgao kwa kila mmoja kiasi gani na
(3) Kiasi gani kiwekezwe kwa mradi mwingine
(4) Kama kuna wanachama wanaojitoa na wanaojiunga wanunue shares kulingana na mtaji unaohitajika
(5) Uwezekano kununua ardhi ya kikundi nk
habari naomba msaada wa number zenu
ReplyDelete